Posts

Showing posts from October, 2017

Atimae timu ya Azam kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui. Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.

Image
PAMOJA na kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui. Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.  Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 12 ikiwa na jumla ya michezo sita hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara. Katika mchezo huo bao la Azam FC limefungwa dakika ya tisa na nahodha Himid Mao "Ninja" kwa njia ya mkwaju wa Penalti baada ya beki wa kushoto Bruce Kangwa kuangushwa ndani ya eneo la hatari. Azam ingeweza kujipatia mabao zaidi ya mawili katika kipindi cha kwanza kama mshambuliaji wake chipukizi, Yahya Zayd na Mbaraka Yusuph wangekuwa makini kutumia nafasi takribani tatu za kufunga mabao.

BEKI wa Yanga Andrew Vicent "Dante" amesema kwa sasa safu yao ya ulinzi ipo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na kwamba makosa ya mchezo wa Jumamosi hayatajirudia tena.

Image
BEKI wa Yanga Andrew Vicent "Dante" amesema kwa sasa safu yao ya ulinzi ipo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na kwamba makosa ya mchezo wa Jumamosi hayatajirudia tena.  Dante amesema wakati huu anaocheza na Kelvin Yonda amejikuta wakifanikiwa kuelewana kwa haraka ambapo hakuna mshambuliaji anayewasumbua.  Dante alisema Yondani ni moja kati ya mabeki bora na wakongwe ambapo tangu ameanza kucheza naye amejifunza mengi juu ya utulivu wa kuwakabili washambuliaji.  Alisema mkakati wao wa sasa ni kuhakikisha wanamaliza mechi bila kuruhusu wavu wao kutikiswa, mkakati ambao utaanza katika mchezo dhidi ya Stand Jumapili ijayo.  “Ligi ni ngumu lakini kwa sasa sisi mabeki tumekuwa na msimamo mkubwa kwamba hatutaki kuona tunaruhusu mabao tunataka kuona kila mchezo tunatoka tukiwa safi hicho ndicho tulichopanga,” alisema Dante

Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.

Image
Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu. Hayo yamesemwa jana Jumatatu Oktoba 16, 2017 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima mjini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi yanayoratibiwa na kuendeshwa na NEC. Kailima alisema wapiga kura hao wataruhusiwa kutumia vitambulisho vya uraia vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), hati ya kusafiria na leseni ya udereva. “Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia kifungu namba 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambacho kinasema mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari atakwenda mwenyewe kwenye kata aliyojiandikisha, kwenye kituo alichopangiwa, kumridhisha msimamizi wa kituo au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwamba yeye ndiye mpiga kura kwa kumuonyesha kadi ...