Posts

Showing posts with the label HABARI/NEWS

Hatimaye timu ya F stars kuiyaidhibu timu ya KIITEC stars ya jijini Arusha kwa magoli 4-2

Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Fanikiwa stars  imeibuka na ushindi mzito wa mabao manne kwa mawili  (4-2)  dhidi ya timu ya chuo cha mawasiliano na kompyuta  Kiitec united katika uwanja wa chuo hicho uliopo maeneo ya Moshono jijini Arusha. Mchezo huo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza kihistoria siku ya Ijumaa ya tarehe  08 February 2019 , katika dimba hilo la Moshono na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa timu zote mbili huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo. Mchezo ulianza kwa kasi ya aina yake huku  Fanikiwa Stars  wakiongoza kwa kulishambulia kwa kasi lango la timu ya  Kiitek United  na baada ya dakika chache tu baada ya mpira kuanza, mchezaji wa Fanikiwa Stars alichezewa rafu katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo  Patrick Temba akaamuru penati ipigwe na  Fanikiwa Stars  kuandika bao la kwanza, hadi kipindi cha kwanza kuisha Fanik...

Kusaga aacha ujumbe mzito msiba wa Kibonde ‘vijana tuache nyodo, kama uhai ni pesa basi watu wetu wasinge kufa”

Image
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga a metoa ujumbe mzito katika salamu za Clouds Media wakati wa mazishi wa mfanyakazi wao, Kibonde aliyefariki akiwa mkoani Mwanza akipatiwa matibabu. ” Hakuna msanii Mkubwa na maarufu zaidi ya Ruge wala zaidi ya Kibonde kwa hapa Tanzania. Hakika tuache majivuno ulimbukeni wa mali umaarufu na Madaraka Kwani hivi vyote ni vyakupita na tutaviacha Hapa Hapa Duniani. Kama UHAI ungekua ni pesa basi watu wetu wasinge kufa maana tungetafuta pesa kwa namna yeyote ili ili ndg zetu wapone. Lakini hakuna Mtu yeyote Duniani mwenye uwezo wa kununua UHAI wala kuzuwia Mauti. Vijana tupendane sana sana na tuache kujivuna na kujiskia”- Mkurugenzi Mkuu Clouds Media Group’ Joseph Kusaga J Kusaga. RIPkibonde chanzo    BONGO 5

Serikali ya Tanzania yatishia kuufunga mgodi wa Acacia Tarime

Image
Waziri wa Madini Doto Biteko ametishia kuufunga mgodi wa ACACIA North Mara ifikapo Machi 30 mwaka huu, endapo utashindwa kudhibiti maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya watu. Waziri Biteko ameyasema hayo baada kushuhudia kiasi kikubwa cha maji hayo yakielekezwa kwenda maeneo ya wananchi. Tshisekedi na Kabila watangaza serikali ya Muungano R Kelly avunja ukimya Je Mbowe na Matiko wataachiliwa leo? Je, siri za watumiaji wa Facebook zitalindwa kweli? Akizungumza baada ya kukagua miundo mbinu ya maji machafu katika mgodi huo, siku ya Jumanne, waziri huyo ameutaka mgodi huo kuhakikisha tatizo la maji linapatiwa ufumbuzi kabla ya tarehe 30 mwezi Machi. ''Serikali haitajali muwekezaji, sisi maisha ya Mtanzania hata mmoja ni muhimu mno, nyie kwa kuwa mnafanya biashara, mnatakiwa kuzingatia usalama wa watu hapa'' Alisisitiza waziri Biteko. Kwa mujibu wa waziri Biteko, tayari serikali imekwishatuma timu ya wataalamu kukagua mgodi huo, na kwamba wamekwishapewa mu...

Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila waamua kuunda serikali ya muungano

Image
Kiongozi mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamesema wameamua kuunda serikali ya muungano kufuatia mazungumzo, shirika la habari la AFP linaripoti. Licha ya ushindi wa rais Tshisekedi -- kiongozi huyo amejikuta akilazimika kugawanya uongozi tangu uchaguzi huo wa urais. Mpaka sasa hajafanikiwa kumteua waziri mkuu kutokana na kwamba muungano wa Kabila - Common Front for Congo (FCC) una uwingi katika bunge la taifa. Je Mbowe na Matiko wataachiliwa leo? Je, siri za watumiaji wa Facebook zitalindwa kweli? R Kelly avunja ukimya Mgomo wa wafanyikazi JKIA ulikuwa na athari gani? Mkwamo huo umeweka kizuizi kwa maazimio ya Tshisekedi kuigeuza nchi hiyo inayogubikwa kwa rushwa na tuhuma za ukiukaji wa haki za binaadamu. Katika taarifa ya pamoja hapo jana Jumatano, Tshisekedi na Kabila wamesema kwamba licha ya "FCC kuwa na uwingi mkubwa bungeni" katika kuidhinisha matakwa yalioelezewa na wapiga kura, FCC na CACH wa...

Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington.

Image
Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington. Kiongozi huyo alipewa mwaliko wakati wa mkutano wa historia baina ya wawili hao nchini Singapore Jumanne. Kim pia alimwalika pia Trump kutembelea Pyongyang. "Viongozi ao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja," shirika la KCNA limeripoti. Kenye tamko lake la kwanza kabisa tangu kutokea kwa mkutano huo, Bw Kim amenukuliwa akisema kwamba kuna haja ya "dharura" ya kusitisha "hatua za kijeshi za uchokozi zinazokera kati ya mataifa" hayo mawili. Alisema nchi zote mbili zinafaa "kujitolea kujizuia kufanya uchokozi" na "kuchukua hatua za kisheria na kitaasisi kuhakikisha hilo linafanyika", KCNA wameripoti. Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribi...

Atimaye chama cha mapinduzi ccm kimeombwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kidunia wa viongozi wa vyama vya kisiasa

Image
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeombwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kidunia wa viongozi wa vyama vya kisiasa, maombi haya yamewasilishwa na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba kuonana na Ndg. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Katika salamu zake Balozi Wang Ke ameeleza China na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kinampongeza Ndg. Bashiru na kwamba wako tayari kushirikiana naye katika masuala mbalimbali kama sehemu ya mahusiano ya muda mrefu kati ya Tanzania na China na vyama vya CCM na CPC.  Aidha, Balozi Wang ametumia mkutano huo kuwasilisha ombi la China kwa Chama Cha Mapinduzi kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kidunia wa Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika na unaotarajiwa kufanyika mwezi wa Julai 2018.   Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeichagua Tanzania na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa na wa kihis...

Wanafunzi wawili katika chuo cha UDSM wafariki dunia

Image
Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kupitia Wizara ya Afya imesema kuwa imopokea kwa masikitiko taarifa ya ajali iliyotokea June 11, 2018 maeneo ya Riverside Ubungo Jijini Dar es salaam. Ajali hiyo imehusisha Ambulance ya Chuo na Hiace iliyokuwa na wanafunzi ambao wametambulika kwa majina ya, Soko Maria Godian aliyekuwa anasoma mwaka wa kwanza, Steven .E. Sango aliyekuwa anasoma mwaka wa pili, James ambaye alikuwa dereva wa Ambulance. Hata hivyo, taarifa hiyo ya DARUSO imeeleza kuwa mwanafunzi mwingine Abishai Nkiko aliyekuwa anasoma mwaka wa tatu bado anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali yake bado ni mbaya zaidi.

Hatimaye jamii Forum kuto kutowa huduma inchini

Image
Jukwaa maarufu nchini Tanzania Jamii Forums limekuwa miongoni mwa watoaji huduma za maudhui mtandaoni ambao wameathiriwa na kuanza kutekelezwa kwa sheria mpya za mtandaoni. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imewataka watu ambao wamekuwa wakitoa imetoa ilani kwa wahudumu wote ambao bado hawajapata leseni kukoma kutoa huduma hizo kuanzia leo. Mamlaka hiyo imesema wahudumu hao wana hadi Ijumaa wiki hii kuhakikisha wamejipatia leseni la sivyo watachukuliwa hatua. Magufuli awatahadharisha wanahabari Tanzania TCRA imesema wanaoathirika ni wamiliki wote wa blogu, majukwaa ya mitandaoni, redio na televisheni. Wameandika kwenye mtandao wao: "Kutokana na notisi iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo Juni 10, 2018 inayotoa muda mfupi wa kututaka kusitisha utoaji huduma mara kabla ya Juni 11, 2018, tunalazimika kutii mamlaka na hivyo huduma hii haitapatikana kwa muda wakati tukifanya jitihada za kuhakikisha huduma inarejea. "Kwa wateja wetu walio nchi ...

Kim Jong-un afanya ziara ya kushtukiza Singapore

Image

Hali ilivyo: Mazishi ya pacha Maria na Consolata Tanzania

Image
Watu wengi wamejitokeza asubuhi ya leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) eneo la Iringa katika ibada maalumu ya kuwaaga pacha waliokuwa wameungana Maria na Consolata waliofariki mwishoni mwa juma. Miongoni mwa waliofika ni viongozi mbali mbali wa dini na kiserikali.Baada ya ibada kutakuwa na maandamano ya kuelekea katika makaburi ya Tosamaganga ambapo ndipo miili yao itakapopumzishwa. Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya Pacha hao vinafaa kutumiwa na Watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu. "Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata." Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani. Vifo vya Maria na Consolata ambao walikuwa ni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ruaha vimegusa wengi hasa kutokana na ujasiri walioonyesha wakati wa uhai wao. Vile vile watakumbukwa kwa ucheshi wao. Pacha hao wameanda...