Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington.

Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington.
Kiongozi huyo alipewa mwaliko wakati wa mkutano wa historia baina ya wawili hao nchini Singapore Jumanne.
Kim pia alimwalika pia Trump kutembelea Pyongyang.
"Viongozi ao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja," shirika la KCNA limeripoti.
Kenye tamko lake la kwanza kabisa tangu kutokea kwa mkutano huo, Bw Kim amenukuliwa akisema kwamba kuna haja ya "dharura" ya kusitisha "hatua za kijeshi za uchokozi zinazokera kati ya mataifa" hayo mawili.
Alisema nchi zote mbili zinafaa "kujitolea kujizuia kufanya uchokozi" na "kuchukua hatua za kisheria na kitaasisi kuhakikisha hilo linafanyika", KCNA wameripoti.Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribio ya mapinduzi ya serikali Korea kaskazini.
Hakuna tarehe iliyotolewa kwa ziara hiyo lakini katika mahojiano na shirika la habari la Fox News, Trump alikuwa amesema baadaye kwamba Kim anakaribishwa kuzuru White House wakati wowote ule utakaofaa.
Hayo yakijiri, Marekani imewahakikishia washirika wake katika eneo la Asia Mashariki kwamba itatekeleza majukumu yake ya kuwalinda.
Hii ni baada ya Rais Trump kukubali kufutilia mbali mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini baada ya kukutana na Bw Kim.
Korea Kaskazini imekuwa ikiitaka Marekani kusitisha mazoezi hayo yanayofanyika kila mwaka kwa muda mrefu.
Uhasama kati ya Marekani na Korea Kaskazini ulikuwa ukizidi kila mazoezi hayo yanapoanza.
Hatua ya Trump kukubali kusitisha mazoezi hayo ilionekana kama 'kubadilisha msimamo pakubwa' kwa Marekani na iliwashangaza washirika wa Marekani katika kanda hiyo.
South Korean and US tanks fire live rounds during a joint live-fire military exercise near the demilitarized zone, separating the two Koreas in Pocheon, South Korea. April 21, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarekani na Korea Kusini huandaa mazoezi ya kijeshi mara kwa mara
Mazoezi hayo ambayo pia huitwa "michezo ya kivita" hufanyika nchini Korea Kusini na kuwashirikisha wanajeshi wa Korea Kusini na wanajeshi wa Marekani walio nchini humo.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alizungmza na Rais Trump kwa njia ya simu baadaye Jumanne, lakini taarifa rasmi iliyotolewa baada ya mazungumzo hayo haikugusia mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi, Reuters wamesema.
Siku iliyotangulia mkutano wa Jumanne, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis alikuwa amewaambia wanahabari kwamba hakuwa anaamini kiwango cha wanajeshi wa Marekani rasi ya Korea kingezungumziwa.
Alipouliwa iwapo angejua kama mazungumzo kama hayo yalikuwa yameandaliwa, alisema, "Ndio, bila shaka ningejulishwa."
A US soldier stands guard in front of the Peace House in the demilitarized Zone between South and North KoreaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKuna maelfu ya wanajeshi wa Marekani Korea Kusini
Presentational grey line
South Korean newspapers reporting the Trump-Kim summitHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMagazeti ya Korea Kusini yameripoti kuhusu mkutano wa Trump na Kim
Mkutano huo wa Jumanne uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ghamu ulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa, Singapore.
Trump na Kim Jong-un walikubaliana nini?
US President Donald Trump (R) shakes hands with North Korea"s leader Kim Jong-un (L) as they sit down for their historic US-North Korea summitHaki miliki ya pichaAFP
Mwandishi wa BBC amedondoa mambo manne makuu ambayo Trump na Kim wameafikiana kwenye waraka wao:
  • Marekani na Korea Kaskazini zitaanzisha uhusiano mpya wa Marekani na Korea Kaskazini kwa mujibu wa matamanio ya raia wa nchi zote mbili ya kuwa na amani na ustawi.
  • Marekani na Korea Kaskazini zitashirikiana katika kujenga na kudumisha amani ya kudumu Rasi ya Korea
  • Kukariri maafikiano ya Panmunjom ya Aprili 27, 2018 wakati wa mkutano wa marais wa Korea Kusini na Kaskazini, kwamba Korea Kaskazini itachukua hatua kuhakikisha kuangamizwa kabisa kwa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.
  • Marekani na Korea Kaskazini zimejitolea kuhakikisha kupatikana kwa mateka wa vita na watu waliotoweka vitani, pamoja na miili yao, ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa wafungwa na miili ya wale waliotambuliwa.
  • TAHARIFA NA BBC

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu