Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Mazishi ya mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Mwimbaji huyo aliyetesa kwa sauti yake tamu na kwa tungo zake za kusisimua, amezikwa katika makaburi ya Kisutu huku idadi kubwa ya wanamuziki wa fani mbalimbali ikiwa sehemu ya umati uliofurika makaburini hapo.
Aidha, Dede pia amezikwa na vigogo wengi wa dini ya Kiislam, maofisa wengi wa serekali na wanamichezo maarufu.
Pengine kwa miaka ya hivi karibuni, ukiondoka msiba wa marehemu Muhudini Gurumo, hakuna tena msiba wa mwanamuziki wa dansi uliohudhuriwa na watu wengi kama huu wa Dede.
Mwili wa Dede ukiswaliwa swala ya mwisho katika msikiti wa Makonde, Kariakoo
Safari ya kuelekea makauburini inaanza
Umati wa watu ukiondoka Kariakoo kuelekea makaburi ya Kisutu
Kila mtu alitamani kubeba jeneza lililobeba mwili wa Dede
Mkurugenzi wa East African Meleody Ashraf Mohamed akiwa na mwanae njiani kuelekea Kisutu
Katikati ni kiongozi wa Msondo Said Mabela
Ras Inno (kushoto) akibadilishana mawazo na Mjusi Shemboza wa Sikinde
Umati mkubwa wa watu ukielekea makaburi ya Kisutu
Jeneza la Dede likiwa katikati ya umati wa watu
Sehemu ya umati mwingine wa watu
Aliyekuwa mwimbaji wa Chumvi Chumvi, Oscar (kushoto) akiwa na Pishuu wa Msondo
Baadhi ya wanamuziki wakiwa nje ya makaburi ya Kisutu wakisubiri mwili wa Dede
Kaburi la Dede kabla mwili haujawasili
Watu wa karibu wa Dede wakiwa ndani ya kaburi tayari kwa kupokea mwili wa Dede
Mwili wa Dede ukiingizwa kaburini
Mazishi yakiendelea
Katikati ni mwimbaji wa zamani wa Msondo Papa Upanga
Katikati ni mwimbaji wa zamani wa Sikinde Bitchuka
Mwenye kofia ni Hussein Jumbe
Baadhi ya waumin walioshiriki mazishi ya Dede
Kulia ni Mohamed Mauji na Omar Teggo kutoka Yah TMK Taarab
Salam kutoka BASATA
Sehemu ya umati uliofurika makaburini
Ama kwa hakika Dede amezikwa na watu wengi
Baadhi wa wanamuziki wakiwa makaburini
Wanamuziki wa dansi na kizazi kipya ...Zahoro Bangwe, Inspector Haroun na Khalid Chokoraa
Hitimisho la mazishi ya Dede
Watu wakipata sadaka ya chakula Karikoo baada ya kutoka makaburini
Comments
Post a Comment