Uamuzi Wa Kikao Cha Kamati Ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini TFF


Kamati ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la soka nchini TFF, ilikutana jana Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kamati hiyo ya utendaji ilikutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.

Katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.

Katika Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.

Katika Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda na wajumbe ni Msomi Wakili  Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na Mohammed Gombati.

Kadhalika katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.

Kamati ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi – ASP Benedict Nyagabona.

Kamati ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Wakili Msomi, Rahim Shaban kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger