BAADHI ya viongozi wa Simba, jana Jumapili waliwatembelea katika Gereza la Keko, rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu


BAADHI ya viongozi wa Simba, jana  Jumapili waliwatembelea katika Gereza la Keko, rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu
Aveva na Kaburu wapo gerezani hapo baada ya kufikishwa Alhamisi iliyopita wakituhumiwa kwa makosa matano ikiwemo la utakatishaji fedha.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ndiyo wamewashitaki viongozi hao ambapo baada ya kusomewa mashitaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Alhamisi iliyopita, walinyimwa dhamana na kupelekwa mahabusu ambapo kesi hiyo itatajwa tena Julai 13, mwaka huu.
Viongozi ambao walifika leo asubuhi kuwaona Aveva na Kaburu, ni Said Tully, Musleh Al Rawah, Haji Manara na Ally Suru.

Comments

Popular posts from this blog

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger

Makaburi kumi yagundurika katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo katika mkowa wa kasai