Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu




KOCHA wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema baada ya kumaliza mafunzo yake ya ukocha kwa sasa akili yote ameihamishia kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara ambapo amepanga kuanza mazoezi Julai 17, mwaka huu.


 Hivi karibuni Mexime alihitimu kozi ya daraja A ya shirikisho la soka Afrika (CAF), iliyofanyika makao makuu ya shilikisho la soka Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku 19. Akizunghumza na sarianews, Mexime alisema alikuwa bize na mafunzo lakini kwa sasa amemaliza hivyo ameanza kupanga program ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.


 “Nataraji kuanza kambi pamoja na mazoezi Julai 17 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kama unavyotambua Ligi inakuwa na ushindani mkubwa hivyo lazima tujipange vizuri,”alisema.


 Akizungumzia kuhusu tetesi za klabu hiyo kumuhitaji mchezaji wa Yanga, Oscar Joshua, alisema hawana mpango wowote wa kuchukua mchezaji huyo kwani tayari walishaweka usajili wao wazi. 


Hadi sasa klabu hiyo imefanikiwa kuwasajili wachezaji Juma Nyoso, beki Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar, viungo Petter Samson, Mwalyanzi, Ludovic Venancev na mshambuliaji Omary Daga Dagashenko pamoja na kipa Hussein kutoka JKT Ruvu.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger

MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini.