Muumini wa kanisa la katoliki Adrian Mpanda amefariki baada ya kupigwa risasi mbili akiwa anasubiri kuingia kwenye ibada katika kanisa la parokia ya kibangu wilaya ya ubungo jijini Dar es salaam





Muumini wa kanisa Katoliki, Adrian Mpande amepigwa risasi mbili akiwa anasubiri kuingia  kanisani katika Parokia ya Kibangu wilaya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa George Ng’atigwa ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa Mpande alikuwa akisubiri kuingia kanisani majira ya saa tatu asubuhi lakini alikuja mtu mmoja aliyekuwa anatembea kwa miguu na kumpiga risasi ubavuni na mkononi, hali iliyosababisha aanguke na kupoteza fahamu.

Alisema kuwa mtu huyo alikimbia lakini watu waliokuwa maeneo hayo walifanikiwa kumkamata baada ya kuishiwa risasi wakati akijaribu kuwatishia.

Aliongeza kuwa baada ya kumkamata mtu huyo, waliwasiliana na jeshi la polisi ambalo lilifika na kuondoka naye kwa ajili ya taratibu za kisheria na kwamba majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika zahanati iliyokuwa karibu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa limetokana na ugomvi wa kifamilia.

“Mtuhumiwa tunaye tunaendelea kumhoji na aliyejeruhiwa yuko hospitali anaendelea na matibatu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,”Kamanda Kaganda anakaririwa.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger