Yanga kukaa kimiya kumepelekea simba kuwa na wakati mgumu katika lango la usajili alisema kocha msaidizi wa simba Jackson Mayanja alisem hayo jana tarehe 17/7/2017
KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema ukimya wa Yanga katika usajili wao wa kimyakimya umekuwa ukiwaweka katika wakati mgumu wakihofia kile wanachokifanya.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mayanja alisema bado hawana taarifa za kina juu ya Yanga kuwa imewasajili wachezaji gani ambapo jambo hilo limekuwa likiwaweka katika wakati mgumu kwa kutojua makali yao.
Mayanja alisema, baada ya Yanga kumnasa Ibrahim Ajib, mambo yao yamekuwa yakifanyika kimyakimya na kuwaweka katika wakati mgumu wakishindwa kutambua makali gani zaidi wamepanga kuyafanya.
Kocha huyo raia wa Uganda amesema Yanga watakutana nao katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo walitaka kujua mapema juu ya undani wa wapinzani wao hao kabla ya kuanza kufanya maandalizi ya mchezo huo.
“Unaona Simba tumeanza mazoezi lakini kwasasa tutatafuta taalifa za kikosi cha wapinzani wetu lakini ugumu tulikutana nao hawa jamaa mambo yao yanafanyika kwa ukimya sana”alisema Mayanja.
“Hatujajua sasa kwamba kikosi chao kitakuwaje tunajua kwamba wamemsajili Ajib lakini bado wachezaji wao wengine hatujawajua hili linatupa wakati mgumu tukishidwa kujua kikosi chao kitakuwa katika muundo upi.
Comments
Post a Comment