Done Deal: Yanga wamemtambulisha Ajib





Ibrahim Ajib ametambulishwa rasmi na klabu ya Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo kwenye mashindano mbalimbali kuanzia msimu wa 2017-2018.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Bonifasi Mkwasa na meneja wa timu Saleh Hafidh wamemtambulisha Ajib mbele ya waandishi wa habari ndani ya makao makuu ya Yanga mtaa wa Jangwani.






Awali zilianza kama tetesi huku Ajib na Yanga wote wakikanusha tetesi ambazo zilikua zikiibuliwa kwamba Ajib amesaini mkataba na Yanga.
Ajib amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na Matheo Anthony, Ajib ameondoka Simba akiwa anavaa jezi namba 23 ambapo kwa upande wa Yanga jezi hiyo inavaliwa na nahodha Nadir Harou ‘Cannavaro’.


Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger

MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini.