KATIBU mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa pole kwa wanachama wa klabu ya Simba kufuatia matatizo yaliyowakumba na kusababisha baadhi ya viongozi wake wa ngazi za juu kufikishwa kwenye vyombo vya dola.


 Baadhi ya viongozi wa juu wa klabu ya Simba ambao wapo mahabusu ni pamoja na rais wake, Evas Aveva na makamu mwenyekiti Geoffrey Nyange “Kaburu”.


 “Sisi wote ni familia ya soka hatuwezi kufurahia matatizo yanayowapata viongozi wa Simba wakati huu, suala hili limetugusa na tunawapa pole wanachama wao.”


 “Hatuna uadui nje ya uwanja, vita yetu ni ya kimpira tu, hivyo yanapotokea matatizo kama haya tunakuwa bega kwa bega katika kufarijiana na kutiana moyo,” alisema Mkwasa. Kesi ya viongozi hao imepangwa kusomwa tena Julai 20, mwaka huu kwenye mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu