Atimae polisi kukatwa mkono



Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarime wakidaiwa kumkata mkono Mkaguzi wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana-River cha nchini Kenya, James Mnuve (50), wakati wakimgombania mwanamke.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kukatwa mkono Mkaguzi huyo wa Polisi wa nchini Kenya. 

Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo. 

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Michael Omahe, anayedaiwa kumtorosha mwanamke huyo, Anne Njeri, kutoka Kenya na kumleta Tanzania kisha kuishi naye kinyumba huku akisaidiana na rafiki yake, Daniel Onchiri.

“Mwanamke huyo (Njeri) anadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pia na askari James Mnuve na walikuwa wakiishi huko Tana River nchini Kenya, baada ya kuondoka, Julai 13 mchana askari huyo alimfuatilia kutoka Kenya hadi Mtaa wa Nkende, Tarime alipokuwa anaishi na kijana aliyemtorosha (Michael Omahe),” alisema Kamanda.

Akaongeza, “Alipofika Mtaa wa Nkende alimkuta Michael, pamoja na rafiki yake huyo wakiwa na mwanamke huyo na hapo ndipo ugomvi ulipoanza kwani askari James alitaka kuondoka na mwanamke huyo na zikazuka vurugu kubwa na kusababisha Mnuve kukatwa kwa kutumia panga.”

Aidha Kamanada huyo alisema kuwa, “Jeshi la Polisi tulifika kwenye eneo la tukio mapema na kuweza kuwakamata watuhumiwa wote watatu; Marandi, Ochiri na mwanamke huyo na kisha tukawahoji kabla ya kuwafikisha mahakamani huku majeruhi akiwa amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibabu.” 

Majeruhi James anadai kuwa yeye ni Inspekta wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana River nchini Kenya na mwanamke huyo, Njeri Wanjoi, ni mke wake.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger