Hatimae kocha wa makipa wa Yanga Juma Pondamali kuwa ameachana na kipa wao Deogratius
KAULI iliyotolewa na kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali kuwa ameachana na kipa wao Deogratius Munishi "Dida" imeonyesha kuwashitua mashabiki wengi wa klabu hiyo.
Wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Dida kuondoka na wengine wakitaka kuvuta subira. Lakini wako mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiutaka uongozi wa Yanga kukaa na kumalizana nae vizuri.
Wengine wameshauri kama amepata timu nje aende lakini sio hapa Tanzania. Pondamali amesema Dida aliwaambia hatasaini mkataba na juhudi za kumbembeleza zimekwama. Hivyo kipa wa Afrikan Lyon waliyomsajili Beno Kakolanya walionaye na watasajili kipa mwingine chipukizi.
Comments
Post a Comment