Atimae kiongozi wa Simba sc Zacharia Hans Poppe amesema wamemtuma mtu kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumsajili Allan Kateregga wa timu ya AFC Leopard


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya simba sc Zacharia Hans Poppe amesema wametuma mtu kwa ajili ya kuzungumza na uongozi wa timu ya AFC Leopard, ili kumsajili mshambuliaji  Allan Kateregga, aliyefanya vizuri kwenye michuano ya Sport Pesa Super Cup
Hans Poppe,  amesema  tangu kumalizika kwa michuano hiyo walikuwa wakijipanga kwa ajili ya kumalizana na wachezaji wengine ambao tayari walishaanza mazungumzo na baada ya kumalizana nao sasa wameona ni muda muafaka kumfukuzia mshambuliaji huyo.
“Ni mchezaji mzuri tumemuona hapa alipokuwa na timu yake ya AFC Leopards, ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza hata eneo la kiungo hata kocha Joseph Omog, alivutiwa naye na ndiyo ametushauri kumsajili,”amesema Hans Poppe.
Kiongozi huyo alisema Kateregga ndiyo atakuwa mchezaji wa mwisho kumsajili msimu huu, na kazi itakayobaki ni kujazia nafasi zenye mapungufu kwa kusajili wachezaji wazawa ambao wataona wanastaili kuichezea timu yao.
Amesema wapo wachezaji ambao tayari walishawaanda kwa kufanya mazungumzo nao ya awali  na hivi karibuni wataanza harakati za kukamilisha usajili wao ili kufunga rasmi zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao.
Simba ilikuwa ikimfukuzi Donald Ngoma wa Yanga, lakini mshambuliaji huyo tayari amewaponyoka na baada  kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Comments

Popular posts from this blog

Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz

Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia

ATIMAE MOHAMED SALAH AVUNJA REKODI YA LIVERPOOL