Geofrey hashingwa kuficha hisia zake kubaini mchezaji mwenzake hata kuwepo kwenye msimu ujao
KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya ameonesha hisia zake kali mara baada ya kubaini kwamba mchezaji mwenzake Haruna Niyonzima hatakuwepo katika kikosi chao msimu ujao.
Niyonzima ambaye ametajwa kusajiliwa na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili, anaachana na Yanga mara baada ya kumaliza mkataba wake msimu uliopita kumalizika.
saria news ilitembelea kwenye mitandao ya kijamii na kushuhudia baadhi ya wachezaji wa Yanga wakionesha hisia zao kuhusu kuondoka kwa kiungo huyo mahariri katika kikosi chao.
Haya ni maneno ya Mwashiuya akimpa maneno ya kwa heri Niyonzima na kumtakia maisha mema katika timu yake mpya.
“Pengo kubwa sana, dah nenda bro wangu Mungu akupe mafanikio mema huko uendako, nakukubali sana chaboli”.
Niyonzima anaondoka akiwa bado ana deni kubwa sana kwa Wana Yanga ambao walikuwa wanaona kama ndiyo mtu ambae alikuwa anajua nini anafanya awapo uwanjani.
Comments
Post a Comment