KLABU ya Everton ya Uingereza ambayo itafanya ziara ya kisoka nchini Tanzania mwezi
KLABU ya Everton ya Uingereza ambayo itafanya ziara ya kisoka nchini Tanzania mwezi huu, imetangaza kumsajili nyota wa Nigeria, Henry Onyekuru ambaye alikuwa kwenye mkopo wa muda mrefu kwenye timu ya Anderlecht.
Taarifa ya klabu hiyo imesema kwamba mchezaji huyo anatua baada ya kuachana na klabu hiyo ya Ubelgiji. Taarifa hiyo imesema kuwa kuwasili kwa Henry Onyekuru kutaimarisha kikosi chao ingawaje pia kuna habari kwamba anaweza kubaki katika kikosi hicho kwa mkopo katika msimu wa 2017/18.
Onyekuru amemaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ujerumani akiwa amepachika mabao 22 katika mechi 38 alizocheza. Lakini sasa Everton imeshinda vita dhidi ya Arsenal na Westham ambazo zilikuwa zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 na amesaini mkataba hadi mwezi Juni mwaka 2022.
Comments
Post a Comment