Atimae taifa stars ya fuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya cosafa
Stars imepata ushindi wake wakati ikicheza dhidi ya wenyeji Afrika Kusini ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa taji hilo.
Maguri amefunga bao hilo pekee dakika ya 18 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Mazamiru Yassin.
Baada ya mchezo, Maguri alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuonesha kiwango kizuri ikiwa ni pamoja na kufunga goli lililoisaidia Stars kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Stars itacheza na Zambia katika hatua ya nusu fainali baada ya Zambia wao kushinda 2-1 mchezo wao wa robo fainali walipo cheza dhidi ya Botswana.
Mechi ya nusu fainali ya Cosafa kati ya Taifa Stars dhidi ya Zambia itachezwa Julai 5, 2017.
Comments
Post a Comment