Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Jeshi la Magereza limefanikiwa kumkatamata Ramadhan Nombo mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutaka kuingiza simu tano kinyume cha sheria katika gereza la Keko wilayani Temeke.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustine Mboje jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni katika gereza hilo.

Alisema Nombo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kuanzia 30 na kuendelea alidakwa wakati akifanyiwa upekuzi katika eneo maalumu la ukaguzi wa wageni mbalimbali wakiwamo wanaowatembelea ndugu na marafiki walioko mahabusu kwenye gereza hilo.

“Huyu (Nombo) alikuwa katika foleni ya mstari wa mwisho ya watu wanaokwenda kuwaaona ndugu zao walioko ndani ya gereza hili. Nadhani hakujua kama sisi kama magereza tuna vifaa vya kisasa vya ukaguzi.

“Ilipofika zamu yake askari wetu walimfanyia ukaguzi na kabla haujaisha kifaa hiki maalumu kiliita alamu kuashiria kuna kitu tofauti,” alisema Mboje.

Alisema alibainika kuwa na simu hizo alizozifunga kitaalaamu na kuficha katika mapande ya nyama yaliyopikwa kwa ustadi wa juu na kuchanganywa na viazi aina ya mbatata.

Mkuu huyo wa magereza, alisema tukio hilo siyo la kwanza katika gereza hilo kwani linatokea katika magereza mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam likiwamo la Segerea.

“Wengine wanatumia hadi mbinu ya kuficha simu hizi katika ugali na mikate lakini tunafanikiwa kuwakamata kutokana na uimara wa vifaa na askari wetu,”alisema Mboje

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger