Polisi Australia washika bunduki ya utawala wa Nazi

Polisi nchini Australia wameshika bunduki ya vita vikuu ya pili ya dunia wakati wa oparesheni kaskazini mwa mji wa Sydney.
Polisi walisaka gari eneo la New South Wales siku ya Jumapili na kupata bunduki hiyo aina ya MP40
Bunduki hiyo ilitengenezwa na utawala wa Nazi nchini Ujerumani ambapo karibu bunduki zaidi ya milioni moja zilitengenezwa wakati huo.
Mwanamume moja wa miaka 40 ambaye alikuwa ni abiria ndani ya gari hilo alishtakwa kwa kumiliki silaha iliyopigwa marufuku.
Australia imeweka sheria kali kwa umiliki wa bundukia. Bunduki ni lazima isajiliwe nakuitumia mtu lazima awe na leseni.
Lakini inakadiriwa kuwa karibu bunduli 260,000 zisizo na vibali ziko nchini Australia.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu