KITENDO cha mashabiki wa klabu ya Yanga kuichoma jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa inavaliwa na kiungo Haruna Niyonzima, kimezidi kupondwa na wanamichezo wengi.
KITENDO cha mashabiki wa klabu ya Yanga kuichoma jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa inavaliwa na kiungo Haruna Niyonzima, kimezidi kupondwa na wanamichezo wengi.
Afisa habari na Mawasiliano wa Simba anayeitumikia adhabu ya kufuingiwa kujishughulisha na soka, Haji Manara amesema kwamba kitendo kinachofanywa na washabiki wa Yanga sio cha kistaarabu.
Manara ameandika katika ukurasa wake wa Instagram akisema kwamba katika miaka ya karibu wachezaji kadhaa wa Simba wamekuwa wamehimaiaYanga, lakini Simba hawajawai kuchoma jezi zao.
“Wenzetu ustaarabu wao ni ziro, iliwajiandae kuchoma nyengine hivi kalibuni,” amesema Manara katika ukurasa wake huo. Manara amesema kwamba wanachofanya Yanga nao wasione ubaya kufanyiwa, akimaanisha kwamba ya Yanga kuwasajili wachezaji wa Simba.
Awali, katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alilani hatua hiyo ya washabiki wa timu yake kuichoma moto jezi hiyo, na kufananisha na upuuzi na kukosa kupevuka kisoka.
“kuhama kutoka timu moja ama nyingine si jambo geni katika soka na Haruna si mchezaji wa kwanza kufanya hivyo. Kuchoma jezi yake ni upuuzi na kuonyesha kushindwa kupevuka katika masuala ya soka.
Matukio haya ni fedheha kwa klabu yetu wenye umiliki wa jezi hizo. Hivyo ningewaomba kuacha mara moja kutulia kufikiria mambo yenye tija” amesema.
Lakini pia baadhi ya washabiki mbalimbali wenye upeo mkubwa wa mambo ya soka wakiwemo hata wale wa Yanga, wamelaani kitendo hicho wakisema kwamba huo ni ukosefu wa shukurani kwa Niyonzima ambaye ameitumikia Yanga kwa miaka sita.
Comments
Post a Comment