Atimae uwanja wa mkwakwani Tanga wafanyiwa marekebisho
UWANJA wa Mkwakwani jijini Tanga unatarajiwa kufanyiwa marekebisho kwenye baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua zilizokuwa zikinyesha sehemu mbalimbali hapa nchini.
Akiongea na sarianews, meneja wa uwanja huo, Nassor Makau amesema ukarabati huo umelenga maandalizi mapya ya Ligi ya Mkoa ambayo yamepangwa kufanyika uwanjani hapo.
“Kama unavyojua, hivi sasa tuko kwenye maandalizi ya Ligi ya mkoa wa tanga, hivyo tunatakiwa kukarabati maeneo ya uwanja, hasa eneo la ardhi kwa lengo la kuuweka kwenye hali nzuri ya kuchezewa,” alisema Makau.
Alisema, wataendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha uwanja huo unakarabatiwa kila wakati ili kutumiwa na klabu zinazoshiriki Ligi mbalimbali, ikiwemo ile ya daraja la kwanza.
Comments
Post a Comment