Shambulio la mjini London ni shambulio dhidi ya Ulaya
Mtu mmoja aliendesha gari na kugonga kundi la waumini wa Kiislamu mjini London, na kusababisha mtu mmoja kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa Uhalifu wake aliofanya ni usaliti kwa maadili ya Ulaya; DW: Kersten Knipp.
Dereva wa gari nyeupe ya kusambaza mizigo ambayo iligonga kundi la Waislamu ambao walikuwa wanatoka tu katika msikiti wao usiku wa Jumapili anafurahishwa kabisa na hatua yake aliyochukua. "Nimefanya wajibu wangu," anaripotiwa kusema hivyo kwa mtu mmoja aliyeshuhudia baada ya kutoka katika gari yake. Jukumu lake : shambulio la kiwoga dhidi ya watu ambao hawakuweza kujitetea waliokuwa wanatoka kutoka katika ibada.
Huenda hatujui mengi kuhusiana na mshambuliaji mwenyewe. Lakini kile tunachojua kwa hakika ni kwamba aliwahi kufanya uhalifu mkubwa kabisa , shambulio dhidi ya watu kwa jumla , ambao wanajitambulisha moja kwa moja na kundi lao. hapa ni , Waislamu. Bila shaka hii ni Chuki na uhalifu , kwa hali isiyoeleweka , na pia ni shambulio la kisiasa ambalo ni chini kabisa ya kiwango chochote cha ustaarabu wa aina yoyote.
Kwa maneno mengine , hili lilikuwa tukio ambalo halina tofauti na shambulio lililofanywa mara kadhaa katika miezi iliyopita na miaka na watu wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu , IS.
Uhalifu wao pia ni wenye sura ya uwoga na uovu tu. Kundi la IS ni kundi linafanya unyama bila kujali maadili ama viwango vya kisiasa.
Mhariri Knipp Kersten
Hii ndio sababu magaidi wanafanya mambo yao kama yule aliyefanya kitendo cha mauaji mjini London ambapo ni kinyume kabisa na msimamo wa kimaadili, na pia ni maafa kwa ustaarabu. Watu wanaofanya mambo kama aliyofanya mshambuliaji huyo na gari yake wako tayari kutumbukia katika kiwango kama cha IS, kiwango cha wakorofi dhalili na walioshindwa maisha, vijana, ambao wanaendeshwa na hamasa , bila kuwa na uwezo wa kudhibiti nafsi zao ama uwezo wa uzalishaji katika jamii.
Nguvu za kibinadamu zinazolisha kundi la IS zimejaa watu wenye hasira duniani kote, watu wenye mtazamo wa uharibifu, hisia za kuuwa na ambao huhisi kuhalalishiwa na propaganda inayotolewa na magaidi wa kundi la IS. Ulaya iliyostaarabika haipaswi kufanya hivyo.
Ndio , Ulaya ni bara ambalo linahistoria ya kumwaga damu. Lakini pia ni bara la ustaarabu. Kanda ambayo , licha ya makosa yote mabaya ambayo inapaswa kuwajibika, uvamizi wa Iraq mwaka 2003 miongoni mwa mengine, kila mara inawajibika na inataka kujifunza kutokana na kujitazama na kujikosoa. Ulaya imeweka kiwango cha juu cha maadili kwake binafsi. Maadili yetu yanataka kwamba tuzungumze baina yetu , na sio kupigana miongoni mwetu na sio kuwafanyia ugaidi wengine kwa misingi ya chuki.
Comments
Post a Comment