Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarime wakidaiwa kumkata mkono Mkaguzi wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana-River cha nchini Kenya, James Mnuve (50), wakati wakimgombania mwanamke. Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kukatwa mkono Mkaguzi huyo wa Polisi wa nchini Kenya. Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo. Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Michael Omahe, anayedaiwa kumtorosha mwanamke huyo, Anne Njeri, kutoka Kenya na kumleta Tanzania kisha kuishi naye kinyumba huku akisaidiana na rafiki yake, Daniel Onchiri. “Mwanamke huyo (Njeri) anadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pia na askari James Mnuve na walikuwa wakiishi huko Tana River nchini Kenya, baada ya kuondoka, Julai 13 mchana askari huyo alimfuatilia kutoka Kenya hadi Mtaa wa Nkend...
Comments
Post a Comment