Qatar yanunua ndege za kivita kutoka Marekani

Qatar imetia saini mkataba wa thamani ya dola bilioni 12 kununua ndege za kivita aina ya F-15 kutoka Marekani.
Biashara hiyo ilikamilishwa katika mkutano mjini Washington kati ya waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatari.
Hatua hiyo inajiri siku kadhaa baada ya rais Donald Trump kuishutumu Qatari ,mshirika mkubwa wa Marekani kwa kufadhili ugaidi wa kiwango cha juu ,madai ambayo Qatar imekana.
Mataifa mengine ya Ghuba hivi karibuni yalivunja uhusiano wao na Qatar wakiilaumu nchini hiyo kwa kuliyumbisha eneo hilo kupitia ufadhili wake wa makundi yenye itikadi kali na uhusiano wake na Iran.
Qatar ndio taifa lenye kambi kubwa ya majeshi ya Marekani katika eneo la mashariki ya kati ,Al-Udeid .


Ramani ya Qatar inayoonyesha nchi zilizokata uhusiano na taifa hilo
Image captionRamani ya Qatar inayoonyesha nchi zilizokata uhusiano na taifa hilo

Kambi hiyo ina takriban wanajeshi 10,000 na ni muhimu katika operesheni za marekani dhidi ya kundi la Islamic state nchini Syria na Iraq.
Matamshi ya rais Trump yalienda kinyume na idara ya ulinzi nchini humo ambayo ilikuwa imeisifu Qatar kwa kuendelea kuimarisha usalama wa kieneo siku chache awali.
Saudia ambaye pia ni mshirika mkuu wa Marekani imeongoza hatua za kutaka kulitenga taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa gesi kuanzia mapema mwezi huu.
Riyadh ilifunga mpaka na anga yake kwa ndege za Qatar Airways huku Bahrain ,UAE na Misri zikivunja uhusiano wao wa kidiplomasia na taifa hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger