FIFA KOMBE LA MABARA: CHILE YAINYUKA CAMEROON!

KWENYE Mechi ya kwanza ya Kundi B ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara iliyochezwa huko Spartak Stadium Mjini Moscow Nchini Russia, Chile wamewafunga Mabingwa wa Afrika Cameroon Bao 2-0.
Mechi hii ilikumbwa na utata wa Maamuzi ya Mfumo wa VARs, Video Assistant Referee, ambapo Refa wa Mechi Damir Skomina wa Slovenia aliesaidiwa na Utaalam wa Video kutoa Maamuzi Mawili ambapo moja alilikataa Bao la Chile kwa Ofsaidi na wa pili kulikubali Bao la Eduardo Vargas.
Bao za Chile zilifungwa mwishoni, Dakika za 81 na 91, kupitia Arturo Vidal na Vargas.
Leo Jumatatu pia ipo Mechi moja ya Kundi B kati ya Mabingwa wa Dunia Germany na Australia.
VIKOSI:
Cameroon: Ondoa; Mabouka, Teikeu, Ngadeu-Ngadjui, Fai; Anguissa, Siani, Djoum; Moukanjo, Aboubakar, Bassogog

Comments

Popular posts from this blog

Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz

Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia

ATIMAE MOHAMED SALAH AVUNJA REKODI YA LIVERPOOL