Urusi yadai kumuua kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdad
Wizara ya ulinzi ya Urusi inachunguza iwapo shambulio lake la angani nchini Syria lilimuua kiongozi wa kundi la Islamic State.
Wizara hiyo imesema kuwa shambulio hilo huenda lilimuua Abu Bakr al-Baghdad na hadi wapiganaji wengine 330 mnamo tarehe 28 mwezi Mei.
Inasema kuwa uvamizi huo ulilenga mkutano wa baraza kuu la Islamic State katika mji wa Raqqa ambao ni makao makuu ya Islamic State kaskazini mwa Syria.
- Kiongozi wa IS asema hawatauachilia mji wa Mosul
- Mshauri mkuu wa kiongozi wa Taleban auawa na Marekani
- Marekani:kupambana na IS ni lengo letu la kwanza
Kumekuwa na idadi kadhaa ya ripoti kuhusu kifo cha Baghdad.
Hii ni mara ya kwanza ,hatahivyo, kwamba Urusi imesema kuwa huenda ilimuua kiongozi huyo wa IS.
Vyombo vyengine vya habari vilidai kwamba kiongozi huyo aliuawa ama amejeruhiwa vibaya kutokana na mshambulio yanayoongozwa na muungano wa Marekani.
Taarifa ya wizara ya ulinzi nchini Urusi iliochapishwa na chombo cha habari kinachofadhiliwa na serikali cha Sputnik imesema kuwa makamanda 30 wa Islamic State na hadi wanajeshi 300 walikuwa katika mkutano huo wa mjini Raqqa, ilongezea.
Kanali John Dorrian ,msemaje wa muungano wa kijeshi unaongozwa na Marekani amesema kuwa Marekani haiwezi kuthibitisha iwapo Baghdad aliuawa.
Hakujakuwa na tamko lolote rasmi kutoka kwa serikali ya Syria.
Uwepo wa Baghdad haujulikani kwa muda mrefu sasa ijapokuwa aliaminika kuwa Mosul nchini Iraq kabla ya majeshi yanayoongozwa na Marekani kuanza juhudi za kuukomboa mji huo mnamo mwezi Oktoba.
Chombo cha habari cha Reuters kiliripoti kwamba anaaminika kuwa katika maficho katika jangwa badala ya kuishi mjini Mosul ama Raqqa.
Kwa mara ya mwisho Baghdad alihutubia hadharani mwaka 2014 Juni alipotangaza uongozi wa kidini mjini Mosul baada ya IS kuudhibiti mji huo.
Comments
Post a Comment