Mabaki ya mji wa kale wa ‘majitu’ yagunduliwa Ethiopia

Wataalamu wa mambo ya kale wamegundua mabaki ya mji wa kale ambao ulikuwa umesahaulika mashariki mwa Ethiopia.
Wanaakiolojia hao wanakadiria kwamba mji huo ulikuwepo kuanzia karne ya 10 na ulikuwa kitovu cha biashara katika eneo hilo.
Kugunduliwa kwa mabaki ya mji huo wa Harlaa kumefichua kuwepo kwa vitu, bidhaa na vifaa kutoka maeneo ya mbali kama vile Misri, India na China.
Miongoni mwa vitu vilivyogunduliwa eneo hilo ni msikiti ambao inakadiriwa ulijengwa karne ya 12, pamoja na makaburi ambayo yalitumiwa na Waislamu waliokuwa wanaishi eneo hilo.
Mwanaakiolojia mkuu anasema muundo wa msikiti huo unafanana sana na misikiti iliyogunduliwa kusini mwa Tanzania na maeneo ya Somaliland, na ni ishara wkamba kulikuwa na uhusiano na mawasiliano kati ya jamii za Waislamu barani Afrika.
Wataalamu hao pia wamegundua sarafu za fedha na shaba za karne ya 13 kutoka Misri, pamoja na vito kutoka Madagascar, Maldives, yemen na China.
Wakulima katika eneo hilo wamekuwa wakipata vitu vya ajabu, vikiwemo sarafu kutoka China katika mashamba yao, jambo ambalo lilichangia kuenea kwa dhana kwamba eneo hilo huenda lilikuwa makao ya majitu.
Wanakiolojia hao hata hivyo wanasema hawakupata ushahidi wowote kwamba kulikuwa na majitu eneo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger