Atimae klabu ya as kigali Rwanda imeiomba Simba kumuuzia mshambuliaji wake Laudit Mavugo


KLABU ya AS Kigali Rwanda imeomba Simba kumuuzia mshambuliaji wake Laudit Mavugo ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo.

 Habari ambazo sarianews  inazo zinasema kwamba klabu hiyo imetuma maombi Simba kutaka kuhuzwa  nyota huyo raia wa Burundi.

 Mtandao mmoja umeandika juzi kwamba Mavugo alikuwa amesafiri hadi jijini Kigali kufanya mazungumzo na klabu yake hiyo ya zamani na kwamba alikuwa amekubali kusaini tena mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijawekwa wazi.

 Hata hivyo, Simba kupitia kwa makamu wake wa rais, Geoffrey Nyange Kaburu imesema kwamba Mavugo amekuwa na wasiwasi baada ya kumsajili John Bocco Adebayor, Emmanual Okwi na mpango wa kumsajili Donald Ngoma, huenda akakosa namba katika kikosi hicho. 


Lakini Kaburu amesema kwamba Mavugo bado ni mchezaji wao na ana mkataba wa msimu mmoja zaidi kuendelea kufanya kazi Msimbazi.

 “Mavugo ana mkataba na klabu na bado klabu haijapokea ofa yoyote kutoka popote ikimuitaji Mavugo,” amesem Kaburu. 

Hata hivyo kuna habari kwamba timu hiyo ya Rwanda imekuwa katika mawindo makubwa ya kumsajili Mavugo, ingawa wana wasiwasi kwamba huenda Simba ikawapiga pesa ndefu zaidi.


 Mtandao huo wa Inyarwanda, umeandika kwamba Mavugo anataka kuondoka Simba kwasababu anajiona kwamba hatakuwa na namba mbele ya Bocco na Okwi.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu