kuna kila dalili simba kuwa moto wakuotea mbali baada wakitaka kumsajili mchezaji kutoka zambia
KUNA kila dalili kikosi cha Simba msimu ujao kikawa moto wa kuoteambali, has baada ya kuripotiwa kutaka kumnasa kiungo fundi mithili ya Haruna Moshi “Boban”, Michael Chaila raia wa Zambia.
Inasemekana Chaila ana uwezo mkubwa wa kusimama juu na mipango hiyo ya kumleta Msimbazi inafanywa kwa siri ili isije kuharibika, Chaila ni mchezaji wa Zesco United ya Zambia, timu ambayo alikuwa akichezea straika mwingine wa Simba, Juma Luizio “Ndanda.
” Inasemekana kiungo huyo mwembamba ana mashuti makali na mwepesi kubadili mchezo, kwa watu wanaomfahamu wanasema Chaila ni zaidi ya Niyonzima na ujio wake unakuja baada ya dili ya kumpata Niyonzima kukamilika.
Simba bado inaendelea kufanya usajili ukiwa na maana ya kukiboresha kikosi chake ambacho msimu ujao kitashiriki michuano ya kimataifa na tayari wameshasajili wachezaji sita wapya ambapo inajiandaa kutambulisha wengine.
Waliosajiliwa na Simba hadi sasa ni Jamal Mwambeleko, Yusuph mlipili, John Bocco, Shomary Kapombe, Emmanuel Elias Mseja na Ally Shomary na huku pia ikidaiwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa Aishi Manula na Waltel Bwalya ama Donald Ngoma kulingana na mahitaji ya kocha mkuu Mcameroon, Joseph Omog.
Comments
Post a Comment