Watu 6 wafa maji na wengine 16 hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama maji inchini colombia


Msako na shughuli za uokozi zinaendelea

Idara ya polisi nchini Colombia, imesema kuwa yamkini watu 6 wamefariki ika ajali ya kuzama kwa boti moja la abiria katika bwawa moja, katika mji mmoja ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Watu 16 hawajulikani waliko, baada chombo cha ghorofa nne, lilipoanza kujaa maji mara tu lilipo n`goa nanga katika ziwa moja la kujiundia, karibu na mkahawa mmoja maarufu kwa watalii la Guatapé, kilomita 45 mashariki mwa Medelini, siku ya Jumapili.

Kulikuwa na watu 150 ndani ya chombo hicho.
Maandamano nchini Colombia

Kwa mjibu wa mtu mmoja aliyeshuhudia ajali hiyo, Juan Quiroz, ameiambia BBC kuwa, chombo hicho kilichukua chini ya dakika 5 kuzama.

Walio okolewa wam,etamaushwa na ajali hiyo

Maboti mengine madogo madogo yalifika kwa kasi na kuanza kuwaokoa watu kutoka majini na orofa ya juu ya chombo hicho.

Aidha, ndege za helikopta na wapiga mbizi wa kijeshi wameonekana mahali pa mkasa huo wakijaribu kuwaokoa manusura.
Mapigano kusitishwa rasmi Jumatatu Colombia

Hakujatolewa taarifa zaidi ya kilichosababisha chombo hicho cha majini kuzama.

"Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi," afisa mmoja wa serikali katika eneo hilo amewaambia wanahabari.

Zaidi ya watu 20 wamekimbizwa hospitalini katika mji wa Guatapé.
Ramani inayoonyesha mji wa Guatape


Luis Bernardo Morales, kapteni mmoja wa idara ya zima moto ambaye anahusika moja kwa moja katika shughuli za uokoaji, amesema kuwa boti hilo lilikuwa karibu na bandari pale lilipozama.

"Hatujafahamu kama kiini cha ajali hiyo ilikuwa ni matatizo ya kimitambo, ubeba watu kupita kiasi au mawimbi ziwani," Shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema.
ELN:tutaachia mateka nchini Colombia

Guatapé ni eneo maarufu kwa watalii katika mji wa Andean, unaojulikana kwa michezo mingi ya majini na sehemu ya burudani.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger