Ndege ya kijeshi ya Urusi yaitishia ile ya Marekani Baltic

Ndege ya Urusi ilipaa futi tano juu ya ndege ya ujasusi ya Marekani katika anga ya bahari ya Baltic siku ya Jumatatu, kulingana na maafisa wa Marekani.
Hatua hiyo ilionekana kuwa isio salama kutokana na kasi ya ndege hizo mbali na udhibiti mbaya wa ndege hiyo, maafisa hao walisema.
Lakini Urusi imepinga malalamishi hayo ya Urusi ikisema kuwa ndege hiyo ya Marekani iliichokoza ndege yake.
Siku ya Jumatatu Urusi iliionya Marekani kwamba ndege za Marekani zinazopaa juu ya ngaa ya Syria zitalengwa.tangazo hilo lilijiri ili kujibu kuangushwa kwa ndege ya Syria baada ya kulenga waasi wanaoungwa mkono na Marekani.
Siku ya Jumanne, Jeshi la Marekani liliiangusha ndege isiokuwa na rubani inayomilikiwa na Iran nchini Syria na hivyobasi kuongeza wasiwasi kati ya Washington na Moscow ambayo ni mshirika mkuu wa utawala wa Syria.
Uchokozi huo wa siku ya Jumatatu ulifanyika kilomita 40 kutoka eneo la Urusi la Kalinigrad katika maji ya kimataifa.
Msemaji wa Pentagon Nahodha Jeff David aliambia maripota kwamba:Tulikuwa tukipaa katika maji ya kimataifa na hatukufanya uchokozi wowote.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger

MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini.