Gari lagonga watu kadhaa London

Mtu mmoja ameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya gari kugonga umati wa watu waliokuwa wakitembea karibu na msikiti kaskazini mwa London.
Mwanamume mmoja wa umri wa miaka 48 alikamatwa kufuati kisa hicho.
Polisi wa kupambana na ugaidi wako eneo hilo. Polisi wamelielezea tukio hilo kama la kigaidi
Waziri mkuu Theresa May amekitaja kuwa kisa kibaya akisema kuwa fikra zake ziko kwa wale waliojeruhiwa, wapendwa wao na watoa huduma za dharura eneo hilo.
Idara ya kutoa hudum za dharura mjini Lanodn imesema imetuma huduma kadha eneo hilo.
Video iliyowekwea katika mitandao ya kijamii ilionyesha vurugu huku watu wakiwasaidia wale waliojeruhiwa.
Tayari mtu moja amekamatwa kufuatia shambulio hilo lililotokea katika wilaya ya Finsbury Park.
Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza tu kuswali swala ya jioni baada ya kuumaliza mfungo wa siku wa Ramadhan.
Video zilizotumwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu walio katika taharuki, kuhu wakijaribu kuwasaidia majeruhi.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu