Madiwani na Naibu Meya CHADEMA Watiwa Mbaroni Arusha

Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Likindikoki, pamoja na madiwani wengine wawili wa Chadema wamekamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika.

Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema Viola pamoja na madiwani hao wawili walikamatwa  jana Alhamisi  wakiwa katika mkutano wa ndani uliokuwa ukisikiliza kero za wananchi.

“Nipo Tanga kikazi na nilimkaimisha nafasi yangu Viola, kwa kawaida Alhamisi tunasikiliza kero za wananchi, wakati wakiendelea kusikiliza kero ndipo walipokamatwa,” alisema.

Wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni diwani wa viti maalumu (Chadema), Kata ya Ngarenaro Happiness Charles na diwani wa Viti Maalumu kata ya Olorieni, Sabrina Francis.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kwa kifupi kwamba jeshi lake linawashikilia kwa uchunguzi.

Diwani wa viti maalumu (Chadema), Jenipher Lomayan  amesema madiwani hao walikamatwa   jana saa 9 alasiri  wakiwa ndani ya ofisi ya Meya wa Jiji la Arusha wakisikiliza kero za wananchi.

Lomayan, amesema  wakiwa ndani ya ofisi hizo polisi waliovalia nguo za kiraia waliingia na kuwaeleza kwamba wako chini ya ulinzi na wanatakiwa kufika mbele ya makao maku ya jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.

“Wale polisi walitaka kuichukua simu ya Naibu Meya na ndipo madiwani wawili (Sabrina na Happiness) wanaoshikiliwa waliingilia kati na kuwazuia polisi wasimnyanganye simu hiyo na ndipo na wao wakaunganishwa katika tukio hilo,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger