Mwigulu Nchemba Awapa Makavu Wanaompinga Rais Magufuli na Kuwatetea Wezi wa Rasilimali za Nchi

Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha Marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu (makinikia), Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzuia serikali iache kufatilia sakata hilo.

"Wale wenye nia mbaya wametafuta vichaka vingi sana lakini kila kichaka wakijaribu na chenyewe kinayeyuka, walisema tutashtakiwa hivi siku hizi mwizi naye anashtaki aliyemwibia? Kichaka hicho kikayeyuka 

"Mwanzoni walikuwa wanasema mchanga tu hauna kitu lakini hili wala halihitaji shule kujua kama ni mchanga tu hauna kitu hawa watu wangekuwa wanakuja kuchukua mchanga tu kila siku. Kwa hiyo hawa watu walikuwa wanatuona kama mazuzu tu lakini Rais wetu amechukua hatua tena si kwa maneno kwa vitendo tumuunge mkono".

"Walipoona kichaka hicho kimekwama wakaanza kutaja viongozi kuwa wanahusika wakidhania hiyo itakuwa kitu cha kuzuia ili jitihada hizo zisiendelee wakaanza kutaja na viongozi wastaafu hiyo yote si kama walikuwa wanataja kuwa viongozi hao wanahusika bali walikuwa wanataka itumike kama kichaka kwamba tukitaja viongozi hao wataacha.

"Mimi niwaambie viongozi wetu hawa hawajawahi kuwa Ma- Agent wa wale wanaotuibia bali wale wanaotetea wezi ambao tumewaona ndiyo Ma- Agent wa wezi hao, na Rais akauona huo mtego akautegua sasa hivi kama ni gari lao lile basi matairi yote Rais Magufuli ameshatoa upepo, yameshalala chini" alisema Mwigulu Nchemba.

Waziri Mwigulu aliyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa ya Ndago katika mwendelezo wa ziara jimbo kwake Iramba Magharibi kuongea na wananchi kuwaeleza alipofikia kuhusu ahadi ambazo walikubaliana kutekeleza hasa suala la umeme kutokufika katika vijiji vingi akieleza kuwa sababu ni mkandarasi aliyekuwepo mkoa wa Singida aliyetolewa baada ya kushindwa kazi lakini sasa ameambiwa na watu wa wizara ya nishati kuwa wakandarasi wawili wameshapatikana hivyo kuanzia sasa zoezi la kuunganisha umeme vijijini utaendelea kwa kasi hasa wa REA awamu ya Tatu.

Kuhusu ujenzi wa zahanati alisema mpaka sasa zahanati katika vijiji vingi alipopita zimefika hatua nzuri ya kupaua na kuwahidi kuwa pelekea mabati na mbao na mifuko ya saruji 100 ili zahanati hizo zikamilike na kuanza kutoa huduma mapema sana.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu