Rais Magufuli afuturisha wananchi wa Pwani, atoa ujumbe kwa waislamu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana  tarehe 21 Juni, 2017 amefuturisha wananchi wa mkoa wa Pwani na kuwataka waumini wa dini ya Kiislam na madhehebu mengine kuendeleza umoja na mshikano uliopo kwa muda mrefu kwa lengo la kudumisha amani nchini.

Mhe. Rais Magufuli alisema anaungana na waumini wa dini ya Kiislamu nchini katika kumi la mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuwaombea kumaliza kwa amani ibada ya Funga ya Ramadhani ikiwa ni kutekeleza nguzo ya nne kati ya nguzo tano ya dini ya kiislam.
 
Alisema kwa mujibu wa dini ya Kiislamu ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni muhimu kwani ni njia sahihi ya kujirekebisha kuachana na matendo maovu yanayoweza kusababisha kutenda dhambi.

‘’Ramadhani ni ibada muhimu kwa Waislaam kwani ndio mwezi ambao huchoma dhambi zao na kutenda matendo mema hivyo ni muhimu kwa ndugu Waislaam kuendeleza yote mema ambayo wanafanya katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuliombea Taifa.’’

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu