CHELSEA ‘MWENDOKASI’ KUWANASA ALEX SANDRO, TIEMOUÉ BAKAYOKO KUMPOZA ‘MBOGO’ CONTE!

MABINGWA WA ENGLAND Chelsea wanatarajiwa Wiki hii kuongeza kasi ya kuwanasa Alex Sandro wa Juventus na Tiemoué Bakayoko wa AS Monaco ili kumtuliza Meneja Antonio Conte ambae amepandwa na hasira kwa kutonunuliwa Mchezaji yeyote Mpya katika Walengwa wa Listi yake.
Conte, ambae yuko Vakesheni huko kwao Italy, alichukizwa na kutokuwepo na jitihada zozote na kukazuka habari ataondoka Chelsea kitu ambacho Klabu hiyo imekikana.
Inadaiwa Chelsea ilimtaka Conte auze baadhi ya Wachezaji waliokuwepo ilia pate Wapya na hilo likamsukuma kumtumia SMS Diego Costa kuwa hayumo kwenye mipango ya Chelsea na kumfanya Fowadi huyo alipue taarifa hiyo hadharani na kuibua msuguano mwingine kati ya Conte na Uongozi wa Chelsea.
Pengine hilo la kuondoka kwa Costa ndilo limewafanya Everton, wakijua wazi Chelsea wanamtaka Straika wao Romelu Lukaku, kudai Dau la Rekodi ya Dunia kumnunua Fowadi huyo wa Belgium alieazimwa toka Chelsea na kisha kuuzwa moja kwa moja kwa Bei chee.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu