Mazishi ya mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Mwimbaji huyo aliyetesa kwa sauti yake tamu na kwa tungo zake za kusisimua, amezikwa katika makaburi ya Kisutu huku idadi kubwa ya wanamuziki wa fani mbalimbali ikiwa sehemu ya umati uliofurika makaburini hapo. Aidha, Dede pia amezikwa na vigogo wengi wa dini ya Kiislam, maofisa wengi wa serekali na wanamichezo maarufu. Pengine kwa miaka ya hivi karibuni, ukiondoka msiba wa marehemu Muhudini Gurumo, hakuna tena msiba wa mwanamuziki wa dansi uliohudhuriwa na watu wengi kama huu wa Dede. Mwili wa Dede ukiswaliwa swala ya mwisho katika msikiti wa Makonde, Kariakoo Safari ya kuelekea makauburini inaanza Umati wa watu ukiondoka Kariakoo kuelekea makaburi ya Kisutu Kila mtu alitamani kubeba...
Comments
Post a Comment