Onyo limetolewa kwa yeyote atakaye mpinga Rais John Pombe Magufuli kwa atakaye mrudisha mtoto aliye pewa mimba shuleni taharifa hii imetolewa na Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba
Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini hapa.
Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.
"Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama kwa Serikali, "amesema.
Comments
Post a Comment