Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara
Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage ameipongeza Singida United kwa kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa ni pamoja na kununua basi lao binafsi aliambia jana sarianews.
Ilipofika kuhusu Singida United kucheza dhidi ya Simba, Rage amesema Singida hawataweza kuchomoka salama mbele ya mnyama.
“Lazima tuwapongeze Singida United wameanza vizuri na watatupa ushindani, lakini wakikutana na timu yangu ya Simba wajue kipigo watakipata tu,”
“Matayarisho yao yamenivutia hasa kitendo cha kutafuta basi zuri, hapo ndio kwenye uhaifu wa vialabu vingi ambavyo viongozi wetu wanakosa. Singida wanawathamini wachezaji wao, wangeweza kuzitumia hizo pesa kwa ujanja mwingine lakini wameamua kuwatafutia basi zuri la kisasa ambalo wachezaji watatumia.”
Mkurugenzi wa Singida United Festus Sanga amesema, basi hilo limenunuliwa kwa shilingi milioni 350 za Tanzania na watalitumia katika safari zao za ndani na nje ya nchi.
Sanga amesema fedhaimetoka kwenye mfuko wa klabu kupitia wadhamini wao ambapo amezitaja kampuni kama SportPesa, Puma na Oryx kama wadhamini rasmi huku kukiwa na wadhamini saba ambao bado wanaendelea na mazungumzo nao na watatangazwa hivi karibuni kama watafikia makubaliano.
Comments
Post a Comment