MLINDA mlango mkongwe wa klabu ya Juventus Gianluigi Buffon amemshauri mlinzi wake katika timu ya taifa ya Italia Gianluigi Donnarumma kufuata matakwa ya moyo wake na kuachana na kelele anazopigiwa kwa sasa.

Buffon wenye umri wa miaka 39, aliibuka na ushauri huo kwa kinda Donnarumma mwenye umri wa miaka 18, aliyewaudhi mashabiki wa klabu anayoitumikia ya AC Milan baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.
“Donnarumma afuate kile ambacho moyo unataka,” alisema Buffon alipokuwa anahojiwa na Sky Sports. “Nilizungumza naye tukiwa na timu ya taifa kwa takriban robo saa na nikamweleza awe huru kuamua atakalo kwenye soka.
” Hata hivyo Buffon ameweka wazi kuwa hahitaji kuona kinda huyo akichukua ushahuri huo bila kufikiria kwa kina kwani huenda akazidisha hasira za mashabiki wa Milan ingawa angependa kumuona akitua Juventus na kuirithi nafasi yake
Comments
Post a Comment