simba na yanga wapata somo tutoka timu ya everton kwa siku ya jana
Shabiki mmoja ameshindwa kujizuia baada ya kutoka jukwaani na kuingia hadi uwanjani kwenda kumkumbatia star wa Everton Wayne Rooney wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Gor Mahia dhidi ya Everton.
Rooney alikuwa amezungukwa na mabaunsa zaidi ya watatu nje akiwa nje ya uwanja ili kupunguza usumbufu wa watu waliokuwa wakitaka kupiga nae picha ‘selfie’.
Jamaa huyo ambae alikuwa amevaa jezi ya Manchester United hakufahamika jina lake mara moja alikimbia kutoka jukwaani na kukatiza uwanjani hadi kwa Roone na kumkumbatia.
Kwenye mechi hiyo, Rooney amefunga goli lake la kwanza tangu arejee Everton akitokea Manchester United sehemu aliyopata umaarufu mkubwa kutokana na mafanikio aliyoyapata.
Mechi hiyo imemalizika kwa Everton kupata ushindi wa magoli 2-1. Everton walitangulia kufunga goli la kwanza ambalo lilipachikwa na Rooney kisha Medie Kagere akaisawazishia Gor Mahia kabla ya Dowell kufunga bao la pili kwa Everton.
Comments
Post a Comment