MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini.



MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini.

Kila timu imeshaangusha pointi

Ni timu tano tu ambazo hazijapoteza mchezo katika ligi kuu msimu huu. Mtibwa, Azam FC, Simba, mabingwa watetezi Yanga na Tanzania Prisons, lakini zote hizo tayari zimeangusha pointi msimu huu huku Mtibwa na Azam FC wakiwa pekee waliangusha alama chache (mbili) baada ya kila timu kucheza michezo minne.

Simba tayari wameangusha pointi nne, sawa na Yanga na Prisons ambazo zimeshinda michezo miwili na kupata sare katika michezo mingine miwili. Hii inamaanisha ligi imeanza kwa ugumu licha ya washambuliaji kuonekana kuwa na ‘usongo’ wa kufumania nyavu.

Wakati Mtibwa wakiangusha alama mbili Jumapili iliyopita mbele ya Shooting pale Mlandizi, Azam FC wao walibanwa na Simba katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi walipotoka suluhu wiki mbili zilizopita.

Singida United wameangusha alama tatu tu katika michezo yao minne ya mwanzo. Timu hiyo iliyorejea Ligi kuu msimu huu ilichapwa 2-1 na Mwadui FC katika mchezo wa ufunguzi wa msimu ipo nafasi ya tatu katika msimamo nyuma ya vinara Mtibwa na Azam FC kwa tofauti ya alama moja tu.

Simba ilishuhudia vijana wa Mbao wakifunga mara mbili na kuisaidia timu yao kupata sare ya kufungana 2-2 Alhamis iliyopita katika uwanja wa Kirumba, Mwanza. Sare hiyo ni ya pili kwa ‘wekundu hao wa Msimbazi’ baada ya awali kulazimisha suluhu vs Azam FC.

Mabingwa watetezi Yanga waliangusha pointi nne wakati walipolazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Lipuli FC katika uwanja wa Uhuru siku ya ufunguzi na wakalazimika kupambana kuepuka kipigo cha kwanza msimu huu walipocheza na Majimaji FC katika uwanja wa Majimaji, Songea.

Prisons ambao wameonekana kuanza kuinuka tena baada ya kuvurunda msimu uliopita waliangusha pointi nne wakati walipolazimishwa sare ya kufungana 2-2 na Majimaji FC katika uwanja wa Sokoine, Mbeya, na baadae suluhu vs Ndanda FC katika mchezo wa raundi ya tatu ambao pia ulichezwa katika uwanja wa Sokoine.

Timu mbili tu zimeshinda mechi 3 mfululizo

Mabingwa wa miaka ya 1999 na 2000, Mtibwa Sugar ilianza msimu huu kwa ushindi wa 1-0 vs Stand, wakaichapa Mwadui FC 1-0, alafu wakaizamisha Mbao FC 2-1. Mechi zote hizo walicheza katika uwanja wao wa nyumbani-Manungu Complex, Turiani, Morogoro. Mtibwa ndiyo timu ya kwanza msimu huu kushinda michezo mitatu mfululizo ikifuatiwa na Singida United.

Tofauti na Mtibwa ambao walishinda michezo yote ya nyumbani, Singida United ambao walianza msimu kwa kichapo kutoka kwa Mwadui wao wamefanikiwa kushinda game tatu mfululizo katika viwanja viwili tofauti. Waliifunga Mbao FC 2-1 katika uwanja wao wa muda pale Jamhuri, Dodoma, wakashinda 1-0 vs Stand United katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga na wikendi iliyopita walipata ushindi wa tatu mfululizo baada ya kuichapa 1-0 Kagera Sugar FC.

Timu tatu hazijapata ushindi

Washindi wa tatu msimu uliopita, Kagera Sugar wapo katika wakati mgumu hadi sasa. Kikosi hicho cha kocha bora wa msimu uliopita, Mecky Mexime kipo mwishoni kabisa mwa msimamo baada ya kucheza michezo minne pasipo ushindi.

Kagera walianza msimu kwa kuchapwa 1-0 na Mbao FC katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba wanakabiliwa na changamoto kubwa katika ufungaji kwani hadi kufikia wiki ya nne timu hiyo imefunga goli moja tu wakati walipolazimishwa sare na Shooting pale Kaitaba. Katika michezo yao miwili ya ugenini wamepoteza 1-0 mbele ya Azam FC na Singida United.

Majimaji walipoteza mchezo wa pili msimu huu baada ya kuchapwa 1-0 na Njombe Mji FC katika uwanja wa Majimaji Jumamosi iliyopita. Awali walichapwa 1-0 na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda, Mtwara. Sare zao mbili dhidi ya Prisons na ile ya 1-1 dhidi ya Yanga katika uwanja wao wa nyumbani imewafanya mabingwa hao wa zamani wa Tanzania kukusanya alama mbili hadi sasa.

Shooting wanakamilisha orodha ya timu tatu ambazo hazijapa ushindi hadi sasa. Timu hiyo ya Pwani ilichapwa 7-0 na Simba katika wiki ya kwanza, ikalazimisha sare yakufungana 1-1 na Kagera Sugar (ugenini) wakalazimisha suluhu vs Lipuli FC katika uwanja wa Samora na wakicheza game ya kwanza nyumbani waliambulia sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa.

Mtibwa, Singida, Simba, pekee hawajaangusha pointi nyumbani

Mtibwa imefanikiwa kukusanya alama zote 9 katika michezo mitatu walyokwisha nyumbani (Manungu Complex) kama wataendelea kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wanaweza kusumbua msimu huu kwa maana kuna alama 39 wanaweza kuzipata katika michezo 13 (mechi mbili dhidi ya Simba na Yanga hufanyika Jamhuri Stadium, Morogoro.) Uwanja wa nyumbani ni ‘nyenzo’ muhimu kwa timu yenye matarajio ya ubingwa.

Wakati Mtibwa ikishinda kila mchezo pale Manungu, Singida Unite na Simba nazo zimeshinda michezo yote waliyocheza nyumbani hadi sasa. Simba ilishinda 7-0 vs Shooting na wakaichapa 3-0 Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru.

Singida walifunga Mbao FC 2-1, wakasdhinda 1-0 vs Kagera katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Timu hizi tatu ndizo pekee zisizoangusha pointi katika uwanja wa nyumbani hadi sasa.

Prisons haijashinda nyumbani, imeshinda zote ugenini

Licha ya kutoshinda mchezo wowote katika uwanja wa nyumbani, Prisons imefanikiwa kushinda mechi zake zote mbili ilizocheza ugenini huku pia ikiwa timu pekee iliyofunga magoli mengi ugenini. Walianza msimu kwa ushindi wa 2-0 ugenini vs Njombe Mji FC, kabla ya kulazimishwa sare mbili nyumbani na timuza Majimaji FC na Ndanda FC. Wikendi iliyopita wamefanikiwa kuishinda Mwadui FC 3-1 katika uwanja wa Mwadui Complex, Shinyinga.

Kagera, MajimajI, Njombe, Shooting, Mbao hazijashinda nyumbani

Kagera wameshacheza michezo miwili katika uwanja wao wa Kaitaba lakini mechi zote wameshindwa kupata ushindi. Walichapwa 1-0 na Mbao na kulazimishwa sare ya 1-1 na Shooting. Si, Kageratu, bali hata Majimaji FC nao hawajafanikiwa kushinda katika uwanja wa nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Yanga wiki iliyopita, juzi Jumamosi ilichapwa 1-0 na Njombe Mji FC.

Njombe walikaribishwa VPL kwa kichapo cha 2-0 kutoka kwa Prisons pia wakachapwa 1-0 na mabingwa watetezi Yanga. Timu hii ni mpya kabisa katika ligi kuu ya Tanzania bara na wataenda Mlandizi kucheza na Shooting mwishoni mwa wiki hii.

Shooting, Mbao FC nao hawajafanikiwa kushinda mchezo wote ule wa nyumbani, lakini timu hizi zimecheza mara moja tu katika viwanja vyao vya nyumbani. Mbao walilazimisha sare ya kufunga 2-2 na Simba wakati Shooting ikibanwa na Mtibwa na kulazimishwa sare ya 1-1.

Nyavu zimeshatkiswa mara 59

Wakati Simba ikiongoza kwa magoli ya kufunga (12) Kagera na Ndanda FC ndizo timu zilizofunga magoli machache zaidi katika ligi hadi sasa (goli moja) Kila timu ikiwa imecheza michezo minne Shooting inaonekana kuwa na safu ‘isiyotulia’ ya ulinzi ambayo imeruhusu magoli tisa (idadi kubwa zaidi ya magoli ya kufungwa hadi sasa)

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu