Atimae timu ya mtibwa sugar inaongoza lingi ikiwa na pointi 10



Timu ya Mtibwa Sugar inaongoza ligi ikiwa na pointi 10, lakini baadhi ya mashabiki na wadau wa soka wamekuwa wakiibeza timu hiyo kuwa wamewashikia nafasi baadhi ya vilabu.

saria news imemtafuta kocha mkuu wa timu hiyo Zuber Katwila ambaye amesema, wanaoibeza timu yake kuwa wameshika nafasi za watu wasubiri wataona kitakachotokea.

“Mimi mwenyewe nimekuwa nikizisikia hizo taarifa watu wakitubeza lakini wanatakiwa watambue kuwa hii ligi haina mwenyewe, kila timu inaweza kuwa bingwa kwa hiyo kama wataendelea kutubeza bila kufanya vizuri wataona kitakachotokea,” Katwila.

Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi Uhuru, amesema anafanya maandalizi na kikosi chake kama mechi zingine za ligi huku akiongeza mbinu za kumfanya atoke na ushindi.

“Ni mechi ngumu ambayo inaweza kutupandisha ama kutushusha kutokana na pointi zetu zilivyo, lakini mimi na wenzangu tunakiandaa kikosi vizuri kama mechi zingine, tumerudi Manungu kwa ajili ya maandalizi zaidi na ndio maana hatujaweka kambi Dar tunataka utulivu,”.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger