STAA wa muziki wa kizazi kipya, Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz kwa staili ya kumwaga machozi wakati akiwa kwenye mahojiano. Q Chillah alisema kwamba anaguswa na hali ya Chid Benz ambaye alikaa kwenye rehab kwa muda mrefu akitibu tatizo la matumizi ya dawa za kulevya. “Nimeguswa na hali ya Chid Benz na najua nimepitia hali nyingi sana kwenye maisha ambazo Chid pia amepita,” alisema rapa huyo . “Lakini kikubwa kilichoniliza nimewahi kuwapoteza marafiki wakubwa sana ambao niliwapenda, wasanii wenye majina makubwa Tanzania, mtu kama Albert Mangweha “Ngawair” Mwana hiphop ambaye mimi sijawahi kumuona zaidi yake,” alimaliza rapa huyo. Marapa hao Q Chillah na Chid Benz kwa wakati tofauti wote waliwahi kukiri kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.
Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya uchunguzi. "Leo asubuhi (jana) nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu", amesema Bashe.
Jana majogoo wa London klabu ya Liverpool walithibitisha kumsajili winga wa As Roma Mohed Salah ambaye walimtafuta kwa muda sasa kwa dau la euro million 39. Hii sio mara ya kwanza kwa Salah kucheza katika ligi kuu nchini Uingereza kwani hapo mwanzo kabla hajahamia nchini Italia aliwahi kukipiga na timu ya Chelsea. Mohamed Salah amesema ujio wake Liverpool ni tofauti na Chelsea kwani kipindi wakati anaenda Chelsea alikuwa bado mtotomtoto lakini sasa anajiona ni bora zaidi. “Nina uhakika 100% kwamba kila kitu kimebadilika hadi muonekano wangu,kipindi kile nilikuwa na miaka 20 ila sasa nina 24 na nina uzoefu mkubwa zaidi tofauti na hapo mwanzo” alisema Salah. Mkataba wa Salah na Liverpool utamfanyia kila mwisho wa wiki kuweka kiasi cha euro 90,000 huku akikabidhiwa jezi namba 11 na Firminho akipewa jezi namba 9. Usajili wa Mohamed Salah wa euro million 39 umevunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Andy Caroll aliyesajiliwa kwa euro milion 35 ...
Comments
Post a Comment