Peter Msechu atoa maneno wa muache na mwili wake
STAA wa muziki wa kizazi kipya, Peter Msechu amesema kuwa mwili mkubwa alionao hauzuii kufanya lolote analotaka kwenye jamii kwani anaweza kujimudu kwa lolote na hasa kazi yake ya sanaa.
Msechu amedai kuwa anashangaa mara kwa mara watu wamekuwa wakimpigia simu ili kutaka kumpa dawa za kupunguza mwili wake, jambo ambalo amedai hawezi kulifanya katika maisha yake.
“Mwili wangu ni brand ya kibiashara, hivyo siwezi kubadilisha mwonekano wangu kwa sababu ya kuwalidhisha watu wanaonitazama,” amesema Msechu. “Nimekuwa nikipata kazi nyingi kwa sababu tu ya mwonekano wangu, hivyo anaetaka nipungue nadhani hana malengo mazuri na mimi,” aliongeza.
“Watu hawajui aina ya majukumu ambayo nafanya, kuna wakati nafundisha wasanii, matumizi ya sauti na kazi nyingine nyingi za sanaa, nasisitiza mwili wangu hauna tatizo jamani,” alisisitiza Msechu.
Comments
Post a Comment