Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia.
Bardlaye alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.
Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.
Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.
Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii.
"Kijana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo.
"Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake."
Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa.
Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".
Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.

Comments

Popular posts from this blog

Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz

Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia

ATIMAE MOHAMED SALAH AVUNJA REKODI YA LIVERPOOL