Hatimae simba kukusanya matajiri wake kuongezea nguvu katika kipindi hiki cha kuisuka simba kuwa mpya
KLABU ya Simba inawakusanya matajiri wake wote ili kuongezea nguvu katika kipindi hiki cha kuisuka Simba mpya. Baada ya viongozi wakuu wa Simba, Evans Eveva na makamu wake, Geofrey Nyange “Kaburu” kukabiliwa na kesi ya jinai iliyowasabasbisha kuwekwa rumande hadi Julay 13, mwaka huu, baadhi ya wafadhili wa zamani wa Simba wamerejea katika kuhakikisha Simba inasonga mbele.
Habari zilizoifikia sarianews zinasema kwamba mmoja wa matajiri hao ni mfanyabiashara Rahma Al Kharoos maarufu kama “Malkia wa Nyuki” ambaye miaka minne iliyopita alikuwa akiifadhili Simba katika mambo mbalimbali.
Mwanamama huyo anayefanya biashara zake katika nchi ya Asia amedaiwa kuwa anataka kuipeleka Simba katika kambi ya mwezi mmoja nje ya Tanzania mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usajili. “Unajua malkia amesema wazi kwamba baada ya kuona viongozi wana matatizo, yeye amehaidi kuongeza nguvu lakini mchango wake ni katika kuiweka Simba katika kambi iliyotulia na anataka wakakae nje ya Tanzania,” kimesema chanzo chetu.
Habari za uhakika zinasema kwamba mfanyabiashara huyo amejitolea kuiweka Simba katika kamba maalum nchini Oman kwa mwezi mzima na anataka jambo hili aachiwe yeye. “Anataka katika kipindi hiki yeye aigharamie timu kwa mwezi mzima na anataka kuona Simba haiyumbi,” amesema na kuongeza.
“Bahati njema ni kwamba Simba kuna watu wengi wana uwezo kila mmoja anataka kuonyesha namna ambavyo klabu na timu inasonga mbele.”
Comments
Post a Comment