Makaburi kumi yagundurika katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo katika mkowa wa kasai
Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema kwamba imepata zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa Kasai, mahali ambapo vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia.
Mwendesha mastaka wa kijeshi Generali Joseph Ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa Kamuina Nsapu ambao wamekuwa wakipiga vita majeshi ya serikali.
UN yathibitisha makaburi ya pamoja DRC
Zaidi ya watu 500 wauawa DRC tokea mwezi Machi
Zaidi ya watu 3000 wameuwawa DRC tangu Oktoba
Mnamo wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea kila uchao katika mkoa huo, ambapo takriban watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu.
Umoja huo aidha ulinyooshea kidole jeshi la taifa la Kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.
Hata hivyo jopo maalum la uchunguzi wa mauaji hayo iliamua kwamba hakuna uhalifu wowote wa kivitu uliyotekelezwa na kwamba hakuna mapigano yaliyotangazwa rasmi mkoani Kasai.
Inadaiwa baadhi ya wanajeshi hao walinaswa katika kanda ya video wakiwapiga risasi raia ambao hawakuwa na silaha.
Comments
Post a Comment