Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz
STAA wa muziki wa kizazi kipya, Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz kwa staili ya kumwaga machozi wakati akiwa kwenye mahojiano.
Q Chillah alisema kwamba anaguswa na hali ya Chid Benz ambaye alikaa kwenye rehab kwa muda mrefu akitibu tatizo la matumizi ya dawa za kulevya. “Nimeguswa na hali ya Chid Benz na najua nimepitia hali nyingi sana kwenye maisha ambazo Chid pia amepita,” alisema rapa huyo .
“Lakini kikubwa kilichoniliza nimewahi kuwapoteza marafiki wakubwa sana ambao niliwapenda, wasanii wenye majina makubwa Tanzania, mtu kama Albert Mangweha “Ngawair” Mwana hiphop ambaye mimi sijawahi kumuona zaidi yake,” alimaliza rapa huyo. Marapa hao Q Chillah na Chid Benz kwa wakati tofauti wote waliwahi kukiri kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.
Comments
Post a Comment