imebaki siku moja kufika siku ya jumatano kwa kuwasili straika Donald ngoma akisubiriwa nchini akitokea kwao Zimbabwe




WAKATI kesho Jumatano straika, Donald Ngoma akisubiriwa kutua nchini akitokea kwao Zimbabwe, tayari uongozi wa Simba umeshamuwekea mezani mkataba wa miaka miwili.

Ngoma ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Yanga ambayo tayari amemaliza mkataba, msimu ujao anaweza kuvaa jezi za Simba kutokana na timu hiyo kuonesha nia ya dhati ya kuihitaji saini yake.

Mzimbabwe huyo aliyejiunga na Yanga misimu miwili iliyopita, tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na Simba huku ikitaarifiwa kwamba yamekwenda vizuri.

Chanzo cha ndani ya Simba, iliambia sarianews  kuwa baada ya kuwa na asilimia kubwa ya kumnasa Ngoma, tayari wameshaandaa mkataba ili akitua tu asaini.

“Ni kweli Ngoma tunamuhitaji na tayari tumeshaongea nae kila kitu kimekwenda sawa, alisema atawasili baada ya kumalizika kwa Sikukuu ya Idd,”kilisema chanzo hicho.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu